Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jafo awataka Monduli kumchagua Kalanga

15308 Pic+jaf TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Tamisemi), Seleman Jafo amewataka wananchi wa wilaya ya Monduli jijini Arusha, kumchagua mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo, Julius Kalanga ili ashirikiane na Serikali kutatua kero zao.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika kata ya Bwawani kijiji cha Naaralami, wilayani Monduli, Jafo alisema Serikali itazitambua kero za wanamonduli na  itahakikisha wananchi wa Monduli wanaendelea kusaidiwa kuzitatua.

Alisema Serikali imejipanga kutatua kero za maji na katika huduma za afya kuna mikakati ya ujenzi wa vituo vya afya kwa lengo la kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kupata huduma muhimu.

Waziri huyo alisema Kalanga ndiye mgombea ambaye ataweza kuwasaidia kutatua kero zao, kwani anaungwa mkono na wabunge waliowengi wa CCM.

Kwa upande wake, meneja kampeni wa Kalanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia, William Ole Nasha, alisema Monduli wanapaswa kumchagua Kalanga kwa maendeleo na si wagombea wengine kuomba walindiwe heshima.

"Tumekuja kuwaomba kura, mumchague Kalanga kwa sababu ndiye chama chake kina ilani ambayo inatekelezwa sasa, hao wengine hawana ilani na ndio sababu awaahidi kuwaletea maendeleo," alisema.

Naye Mbunge wa Longido, Steven Kiruswa aliomba wananchi wa Longido kumchagua Kalanga kwani, anajua kero zao, ikiwepo za ukosefu wa maji na migogoro ya ardhi.

"Kalanga anajua kero zenu ni kijana wenu ambaye mnaweza kumtuma kuwapelekea kero zenu serikalini na zikatatuliwa haraka," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz