Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jafo awanyoshea kidole wanasiasa kauli za utata

82768 Pic+jafo Jafo awanyoshea kidole wanasiasa kauli za utata

Tue, 5 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuhitimishwa kwa zoezi la wagombea kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vyama vya siasa vimetakiwa kuacha kutoa kauli za utoto na upotoshaji.

Waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo amewataka wanasiasa kuwa makini na kauli zao ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Novemba 3, 2019, Jafo amesema uchukuaji wa fomu umekwenda vizuri katika maeneo mengi na zilipotokea dosari aliagiza hatua zichukuliwe kwa haraka.

“Tunapata malalamiko kutokana na dosari za hapa na pale katika maeneo machache na kwa haraka tunatoa maelekezo kwa wasimamizi na watendaji, kuruhusu mchakato huo kufanyika bila usumbufu,”

“Niwaombe wana siasa kuacha kutoa kauli tata lengo ni moja kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. Pia nivisihi vyama visicheze rafu huko maana kuna malalamiko mengine yanakuja upinzani kwa upinzani wanahujumiana,”

Kuhusu uwezekano wa kuongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu Jafo amesema hakuna mpango huo hivyo wagombea wote wakamilishe zoezi hilo ndani ya muda. “Nawaelekeza wasimamizi wazingatie sheria na kuhakikisha ofisi zinakuwa wazi muda wote, watu wachukue na kurudisha fomu bila kukutana na usumbufu wowote, suala la kuongeza muda halipo,” amesema Jafo.

Chanzo: mwananchi.co.tz