Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JUMA DUNI AFIKA KISIWANDUI KUTOA POLE KWA VIONGOZI WA CCM

Duni.png?fit=770%2C514 JUMA DUNI AFIKA KISIWANDUI KUTOA POLE KWA VIONGOZI WA CCM

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Chama Cha ACT Wazalendo kimesema kifo cha aliyekuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni Pigo kubwa katika taifa na kuwataka Watanzania wote kuwa wavumilivu kipindi choote cha msia

Kauli hiyo ilitolewa na Makamo Mwenyekiti wa chama hicho Juma Duni Haji akiwa katika Afisi Kuu ya CCM iliyopo Kiswandui Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa Pole kwa viongozi wa CCM na Viongozi wake.

Alisema kuondokewa na mwenyekiti na akiwa Rais ni jambo zitoo sana na kusema inahitajika uwepo wa subra miongoni mwa Watanzania na familia na wanaCCM.

Alisema kuwa Rais John Joseph Pombe Maguful alikuwa Rais alyesimama katika majukwaa na kusema wazi wazi kuwa anayaunga mkono na ataendeleza Maridhiano.

“Sasa ni wajibu wetu sisi uliohai kyaendeeza na kuyaenzi ili walioazisha ambao washatangulia mbele ya haki tuwatendee haki” alisema Haji

Duni alisema Viongozi wa CCM jinsi walivyowapokea ni kiasi gani kuonesha kua yale maridhiao yaliosisiwa na Malim Seif pamoja na baadhi vingozi wa CCM yanaenendelezwa na kutekelezwa kwa vitendo.

Alisema kuwa Viongozi wa chama cha Mapinduzi alipofariki aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT wazalendo walifika AFisini kwao Vuga kutoa mno wa Pole.

“Kwa hali hiyo uaona ni kiasi gani maridhiano yanaendelezwa na tumeaambiana kuwa Wazanzibar na watanzania Kwa jumla sisi ni wamoja tuendeleze umoja wetu” alisema Duni.

Alisema kuwa ama raiya wamefiliwa na rais wao wanatoa pole kwa niaba ya chama cha ACT Wazalendo kwa mama Samia Suluhu Hassan pamoja na kutoa polea kwa wanachama wote wa CCM kuondokewa na mwenyekiti wao ambapo ni pigo kubwa kwa Taifa.

Duni Haji alieleza kuwa Wazanzibar ni wamoja na hapana budi kushirikiana hasa katika matukio haya ya misiba ambayo yameshawahi kutokea.

Hata hivyo alisema matukio kama hayo huwa sababu nyengine ya kuwaunganisha wazanzibar na kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na huungana pamja kata kujega tafa.

“Hakuna mtu aliyetegemea kama matukio hayo ya kifo yatatokea akini ni kazi ya mumba haina makosa”  alisema haji.

Kwa upande mwengine Duni alisema kuwa marais waliopo sasa wote ni wapya na wanategemea kuwa na siasa za umoja n mashiriiano kwa maslahi mapana ya taifa.

“Tunampongeza mama Samia kwa kuchukuwa dhamana kubwa na tunategemea kuwa na siasa za marihiano katika ardhi ya Tanzania” alisema

Sambamba na hilo aliwataka watanzania kushirikiana pamoja katika kusitiri kiongozi huyo ambaye alifariki tarehe 17/3/2021.

Mapema Asubuhi uongozi wa ACT wazalendo ukiongozwa na Makamo huyo walifika Wizara ya Habari Zanzibar na kuweka saini zao katika kitabu cha Maombolezo.

Wakati huo huo waliwaomba wananchi wooe wahudhurie katika kuuwaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati John Joseph Pombe Magufuli wakiwawamevaa Barakaowa.

Chanzo: zanzibar24.co.tz