Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JPM aomba kura kwa simu Shinyanga, Rukwa

433d6c20461cdc8cbf43117b70cadc75 JPM aomba kura kwa simu Shinyanga, Rukwa

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amewapigia simu wananchi katika mikutano tofauti mkoani Shinyanga na Rukwa akiwaombea wagombea ubunge kura, hatua iliyopokewa kwa vifi jo na nderemo.

Mkoani Shinyanga, Magufuli alimpigia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa aliyekuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamilangano, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

Kwa upande wa Rukwa, Rais Magufuli alimpigia simu mgombea ubunge wa Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa, Aeshi Hilaly aliyekuwa akihutubia wananchi katika Viwanja vya Ndua vilivyopo Manispaa ya Sumbawanga na kuwasihi wananchi wamchague mgombea huyo.

Akizungumza na Waziri Mkuu, Majaliwa, Magufuli alisema: “Watu wa Ushetu ninawashukuru sana kwa kumpitisha bila kupingwa Injinia Kuandikwa (Elias). Mimi niko Tunduma, nilitamani niwe hapo na ninyi lakini imemtuma Waziri Mkuu aje kuniombea kura.

Yote ambayo atazungumza Majaliwa nimemtuma mimi, nawatakia mkutano mwema.” Alisema ahadi yake aliyoitoa ya kutengeneza barabara ya Ushetu-Kahama iko palepale na kwamba akimaliza uchaguzi atafika kuwatembelea.

“Naikumbuka hiyo barabara ya Ushetu kwenda Kahama, tutaitengeneza kwa kiwango cha lami. Naomba kura zenu pamoja na madiwani wote wa CCM.” Baada ya Rais Magufuli kuzungumza na wananchi, Majaliwa aliwataka wakazi hao wamchague kwa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu.

Kwa upande wake, mgombea wa ubunge wa Ushetu, Kwandikwa alisema wananchi jimboni humo wamepata mafanikio chini ya Rais Magufuli.

Alitoa mfano wa ujenzi wa barabara za wilaya zilizojengwa kwa kiwango cha lami kilomita 1200 kutoka kilometa 400 mwaka 2015.

Chanzo: habarileo.co.tz