Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JPM - Mimi Urais nitashinda tu tena kwa kura nyingi sana

WhatsApp Image 2020 09 16 At 08.14.46 660x400.jpeg JPM - Mimi Urais nitashinda tu tena kwa kura nyingi sana

Thu, 17 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amewahakikishia wananchi wa Kibondo mkoani Kigoma kuwa katika uchaguzi mkuu ujao atashinda kwa kura nyingi kwani Watanzania wa maeneo yote wanamtaka yeye.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 17, 2020, wakati akiendelea na mikutano yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali huku akisisitiza wananchi kumchagulia madiwani na wabunge kutoka chama hicho.

“Nitasikitika sana kama hamtanichagulia Wabunge na Madiwani wa CCM kwa sababbu mimi Urais nitashinda tu tena kwa kura nyingi sana na ninataka niwahakikishie kwa sababu watanzania maeneo yote wanamtaka Magufuli” Dkt. Magufuli

“Naomba wana CCM wenzangu mliokosa nafasi msinunue, kuchaguliwa pia ni mipango ya Mungu, yule mbunge wa Busanda amegombea mara nne, miaka mitano iliyopita nikamteua kuwa DC mwaka huu ndiye anayegombea pale, hata mliogombea mwaka huu msikate tamaa” Dkt. Magufuli 

Chanzo: millardayo.com