Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JPM: Hesabuni kura hadharani

17d86c8e4d608d6ffa57f7b778162326 Mwenyekiti wa CCM Taifa

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amewataka viongozi wa chama hicho wanaosimamia kura za maoni za wanaCCM walioomba kugombea ubunge na uwakilishi, kufanya kazi hiyo kwa uwazi bila mizengwe yoyote ili kila mwenye haki apate haki yake.

Alitoa agizo hilo jana Ikulu Chamwino, Dodoma, baada ya kuwaapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe, makatibu na manaibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na Katibu Tawala.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia alishuhudia wakuu wa mikoa wakiapisha wakuu wa wilaya na baadaye wote walioapishwa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya aliowateua, waliapa kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma. Alisema, anatumaini kwamba viongozi watakaosimamia kura hizo, watasimamia kwa uwazi bila mizengwe ili kila mwenye haki aweze kuipata.

“Na mimi ningetamani sana viongozi wa chama changu ambao watasimamia uchaguzi huu, kura zikishamaliza kupigwa, zikafanyike kama tulivyofanya kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa, zihesabiwe hadharani, anayepata sifuri aipate hapo hapo na anayepata zote iwe hapohapo,”alisema Rais.

Alisema tabia hiyo ya uwazi, itajenga umoja wa WanaCCM, hivyo viongozi wa chama hicho waliopewa dhamana ya kusimamia kura hizo za maoni, wahakikishe kura hizo zinahesabiwa mbele ya wajumbe ili kila mmoja ajue alichopata.

Rais Magufuli alisema jana alikuwa na taarifa kuwa kwa nchi nzima wanaCCM 10,367 walikuwa wamechukua fomu, kuomba kuteuliwa kugombea ubunge, na kati ya hao, waliokamilisha taratibu na kurudisha fomu hizo walikuwa 10,321 na 46 hawakurudisha fomu.

“Haijawahi kutokea kwamba katika chama kimoja wagombea kwenye kiti tu cha ubunge ni 10,367, bado udiwani, na mimi nawapongeza sana wote waliojitokeza”alisema.

Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Tanzania, wabunge wa Bunge la Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wawakilishi kwenye Baraza la Wawakilishi na madiwani utafanyika Oktoba mwaka huu.

Chanzo: habarileo.co.tz