Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilikuwa mlima mrefu kwa ACT-Wazalendo kuupanda

F9f9e994ceff3474452a58779c15aaa1.jpeg Ilikuwa mlima mrefu kwa ACT-Wazalendo kuupanda

Wed, 19 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KWANZA ninapongeza kwa hatua ya chama chake kushiriki kwenye chaguzi ndogo za Muhambwe na Buhigwe, licha kupigwa vijembe na vyama vilivyosusia chaguzi hizo.

Lakini ninashangazwa pale nilipoona taarifa ya Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe akilalamika kwamba amevamiwa na gari za watu wa CCM wakiwa na mapanga na gari zenye kura feki.

Muda mfupi tena baadae akaibuka na kukubali matokeo ya uchaguzi kishingo upande huku akitoa lawama na malalamiko kadhaa.

Zitto alitoa madai hayo muda mfupi baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo kwenye majimbo hayo kuanza kutolewa na kuonyesha chama chake kushindwa vibaya kwenye uchaguzi huo kwenye majimbo yote mawili huku CCM ikiongoza.

Ninachoona ni kwamba madai ya Zitto yalilenga ku-

potosha jamii kwa kuiaminisha kana kwamba chama chake kimehujumiwa. CCM inastahili ushindi kwenye majimbo haya na kwenye kata zote kwa kuangalia namna ilivyoendesha kampeni zake kisayansi na kimkakati.

CCM ilianza kampeni za Muhambwe na Buhigwe kwa kufunguliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyeambatana na mitambo yote ya viongozi wa Makao Makuu wa Chama hicho wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mama Christina Mndeme.

Wengine walikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Oganaizesheni Moudline Costica, Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) Raymond Mwangwala

na Mjumbe wa kamati Kuu na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga.

Baada ya ufunguzi wa kampeni hizo, mitambo mingine ya viongozi wa juu kabisa wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa akina Mama wa CCM (UWT) Gaudentia Kabaka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Erasto Sima, Katibu Msaidizi wa idara ya Itikadi na Uenezi Zakaria Mwansasu, Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Zanzibar na wengine wengi nao wakatia timu Kigoma kuwanadi wagombea ubunge hao wa CCM.

Wakati kampeni hizo zikielekea ukiongoni ndipo kundi kubwa la wabunge wa CCM wa Bunge la Tanzania wakaongeza nguvu nyingine nzito kwenye kampeni hizo. Pia waliingia wa-NEC wa CCM kutoka

Bara na Zanzibar, viongozi wa CCM ndani ya mkoa na wengine wengi ambao nao walifanya kazi kubwa ya kupita kila sehemu kuwanadi wagombea wa CCM usiku na mchana bila kuchoka.

Makamu wa Rais wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Buhigwe kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango alifunga kampeni za CCM kwa kishindo kikubwa cha sera na kuwanadi wagombea wa CCM na kuhitimisha kabisa ushindi wa CCM.

Hapo ilikuwa ngumu sana kwa ACT-Wazalendo kufurukuta huku Zitto akiishia kuwahadaa wapiga kura kwamba chama chake kingetumia helikopta.

Mwandishi ni mchangiaji wa HabariLEO. Mawasiliano yake ni 0657475347

Chanzo: www.habarileo.co.tz