Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilani ya CCM yabeba mkoa wa Lindi

8b98fe35831ba64b05bfc3d380063538 Ilani ya CCM yabeba mkoa wa Lindi

Mon, 26 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ILANI ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 imeubeba mkoa wa Lindi kwa kupata miradi mingi ndani yake.

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati akiwasomea ilani hiyo wakazi wa mji wa Lindi na vitongoji vyake waliohudhuria kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Ilulu, mjini Lindi.

Alisema ilani hiyo inaelezea kufanyika kwa ukarabati wa gati la Kilwa ambalo liko mkoani Lindi.

“Ukurasa wa 88 katika kipengele cha miradi ya reli inayoendelea, kinataja maandalizi ya ujenzi wa reli ya Mtwara – Mbambabay na matawi ya Mchuchuma na Liganga kwa ubia kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP); ukurasa wa 90 Kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa viwanja 11 vya ndege vya Iringa, Njombe, Songea, Lindi, Kilwa Masoko, Tanga, Moshi, Lake Manyara, Singida, Musoma na Simiyu,”

“Ukurasa wa 92 (ii) inaelezea ukarabati wa vituo saba vya hali ya hewa vilivyopo Zanzibar, Mtwara, Kilwa Masoko, KIA, JNIA, Handeni na Morogoro; ukurasa wa 94 (d) inahusu ujenzi wa reli ya Mtwara - Songea - Mbamba-bay na Matawi; Liganga na Mchuchuma (km 1,000) na ukurasa wa 95 (h) inataja ujenzi kwa kiwango cha lami wa viwanja vya ndege vya Iringa, Moshi, Lake Manyara, Tanga, Musoma, Lindi, Kilwamasoko, Njombe, Singida na Simiyu.”

Alisema ilani inalezea utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati ambayo ipo katika hatua za mwisho za makubaliano ikiwemo mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) na Mradi wa Kusindika Gesi Asilia (LNG) Mkoani Lindi ambayo itaongeza ajira kwa Watanzania na mapato kwa nchi.

“Inaelezea kuimarisha usafi wa mazingira na afya za wananchi kwa kujenga madampo saba ya kisasa katika majiji ya Dodoma, Tanga, Mbeya, Kigoma, Mtwara, Mwanza na Arusha na kukarabati madampo mawili katika halmashauri za manispaa za Moshi na Lindi,” alisema.

Majaliwa ambaye yuko mkoani Lindi kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, alitumia fursa hiyo kuwanadi mgombea ubunge wa jimbo la Lindi, Hamida Abdallah na wagombea udiwani wa kata 20 za jimbo hilo.

Akielezea miradi ya bandari na vivuko, alisema serikali iliboresha bandari ya Lindi kwa kufanya ukarabati wa gati kwa thamani ya Sh bilioni 3.1. “Tumefanya ukarabati na ujenzi wa maghala katika bandari za Lindi na Kilwa Masoko ambao umegharimu Sh bilioni 3.2.

Pia Sh bilioni 1.9 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kivuko cha Kitunda ambacho sasa kinafanya kazi, “Serikali inapanga kununua kivuko kingine kipya kwa sababu kilichopo ni cha zamani na imeamua kutengeneza speed boat moja ya kuwalinda.

Kati ya boti saba zitakazonunuliwa, moja kituo chake litakuna ni hapa Lindi,” alisema. Kuhusu sekta ndogo ya gesi, Majaliwa alisema katika azma ya kuwa na mradi mkubwa wa kuchakata gesi asilia (LNG), kampuni za Equinor na Statoil zinafanya mazungumzo na serikali juu ya kuanza utekelezaji wa mradi huu.

“Mazungumzo hayo yapo katika hatua za mwisho. Kwa sasa fidia ya Sh bilioni 5.2 imelipwa kwa walengwa na usanifu wa kimazingira umeshafanyika,” alisema

Chanzo: habarileo.co.tz