Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu hapa Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa Wanawake CCM Pwani

WhatsApp Image 2022 11 18 At 9.jpeg Huyu hapa Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa Wanawake CCM Pwani

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM Mkoa wa Pwani wamemchagua aliekuwa Mbunge wa Viti maalumu Pwani Mhe. Zaynab Matitu Vulu kuwa Mwenyekiti mpya wa UWT Mkoa huo.

Mhe. Vulu ameshinda nafasi hiyo kwa kupata jumla ya kura 320 Kati ya kura 358 zilizopigwa akifuatiwa na Joan Tandau aliepata kura 38 pekee huku wagombea wawili waliokuwa wakiwania nafasi hiyo wakiingia mitini na kupata kura sifuri.

Katika uchaguzi huo idadi ya kura zilizopigwa ni 358 na hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Mhe. Zaynab Matitu Vulu amewashukuru wajumbe kwa Imani kubwa na dhamara waliyompatia ambapo amewaahidi kuendelea kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live