Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huwezi kumtengamisha Rais Samia na Magufuli - Makonda

Makonda Ccm Nsds Huwezi kumtengamisha Rais Samia na Magufuli - Makonda

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

⁠Atoa majibu kwa wanaohoji kwa nini kipindi cha hayati Magufuli umeme haukukatika tofauti na sasa.

"Kusema kipindi cha Hayati Magufuli umeme ulikuwa haukatiki huko ni kumbagua Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa naye alikuwa sehemu ya Uongozi wa Hayati Dkt. John Magufuli...huwezi kumtenga Dkt. Samia na Mafanikio ya Magufuli hata kidogo ni sawa na kumsifia mtu na kusahau waliomfanya mtu yule kupata ile sifa " Alisema Mwenezi Makonda.

Makonda amebainisha kuwa tatizo la umeme ni kuwa na mipango ya mda mfupi katika kutatua changamoto ya umeme.

Akizungumza na Wananchi wa Kilimanjaro, Mwenezi Makonda amesema kuwa ukirudi hata kwenye historia utagundua tatizo lilikuwa linatibiwa kwa mda kisha linarudi tena kwasababu serikali haikuwahi kuwa na mpango wa muda mrefu.

Makonda ameeleza kuwa kutokana na kutokuwa na mpango wa muda mrefu na mahitaji kuongezeka hivyo imepelekea kuona umeme unakatika na mfano sasa hivi tuna megawati upungufu wa megawati 200 maana yake serikali ingetibu kwa kuongeza megawati 300 na tungeona tumetibu na kumbe baada ya miaka kadhaa tatizo lingerudi tena.

Akiendelea kutoa ufafanuzi, Mwenezi Makonda amesema ndio maana Hayati Magufuli na Rais Samia waliamua kutoa fedha kwa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Mwl. Julius Nyerere ambao utaweza kuzalisha megawati 2115 ili kutibu tatizo hili la kukatika kwa umeme na kazi hiyo inaendelea chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Huu muendelezo wa ziara yake katika mikoa 20 Back To Back

Chanzo: www.tanzaniaweb.live