Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hotuba ya Sugu imesikilizwa Mahakamani kwa takribani Dakika 39

1886 SU

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa  Emmanuel Masonga wanaokabiliwa na kesi ya kutoa maneno ya kumfedhesha Rais John Magufuli wanatarajia kuanza kujitetea kesho katika Mahakama ya Wilaya Mbeya.

Hatua ya kujitetea kwa washtakiwa hao, inakuja baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao leo.

Wakili wa Joseph Mbilinyi ameieleza Mahakama kuwa wanatarajia kuwa na mashahidi saba na vielelezo nane.

Kesi hiyo ilisikilizwa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Michael Mteite ambaye awali aliruhusu sauti ya hotuba iliyorekodiwa na shahidi wa serikali Inspector Joram Magova isikilizwe Mahakamani.

Sauti hiyo iliyokuwa katika Tape Recorder ilisikilizwa Mahakamani hapo kwa dakika 39.

Baada ya kusikilizishwa sauti hiyo, upande wa mashtaka ulifunga ushahidi ambapo kesi imeahirishwa hadi January 25, 2018 kwa ajili ya Joseph Mbilinyi kuanza kujitetea.

SHERIA INASEMAJE KWA ALICHOFANYA NABII TITO ???

Chanzo: millardayo.com