Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa sababu za Slaa kutofika kwenye Kamati ya Maadili

SLAA Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga

Fri, 27 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutopewa hati ya wito ni miongoni mwa sababu zilizotajwa na mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa ashindwe kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuendelea na shauri la tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Sababu nyingine alizotaja ni kufiwa pamoja na kuugua jambo ambalo amedai kuwa, isingekuwa rahisi kwake kuhudhuria shauri hilo.

Akizungumza mara baada ya kutoka kwenye kikao hicho leo Ijumaa Agosti 27 2021, Silaa amesema alipohojiwa kwa mara ya kwanza Agosti 24, 2021 alimaliza utetezi wake.

“Kamati niliijulisha siku hiyo hiyo ya Jumanne asubuhi kuwa nilifiwa na kwa hali ya kawaida ningeomba hudhuru nisije niliona kwa picha ninayoiona hapa hata ningewaambia wasingenielewa,”amesema.

Pia, amesema suala lingine ni kiafya na kwamba alikuwa asafiri kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mazishi na kwamba, kama ilivyo kwa wengine hata yeye aliona wito wa kuitwa kupitia kwenye mitandao.

“Sikuwa nafahamu kuhusu wito huu, lakini baada ya kuona kwenye mitandao na kwa kuheshimu kamati hiyo niliona ni vyema nifike,” amesema Silaa ambaye ameingia kwenye kamati hiyo saa 4.59 asubuhi na kutoka saa 5:06 asubuhi kisha akaitwa tena 5.27 asubuhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live