Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Heche apitisha bakuli ujenzi ofisi ya CHADEMA

Heche Pic Data Heche apitisha bakuli ujenzi ofisi ya CHADEMA

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche ameahidi kuchangia Sh2 milioni kusaidia ujenzi wa ofisi ya chama hicho Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Heche ametoa ahadi hiyo mjini Sengerema leo Jumatatu Novemba 14, baada ya kupokea taarifa ya Katibu wa Chadema jimbo la Sengerema, Paskazia Renatus kuhusu mpango wa kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya chana wilayani humo.

"Nawapa changamoto wa kujichangisha kupata zaidi ya Sh1.6 milioni za kununua kiwanja; na mkishakinunua mimi natawaunga mkono kwa kuchangia Sh2 milioni ili kuanza ujenzi," amesema na kuahidi Heche

Ahadi hiyo ya mbunge huyo wa zamani wa Tarime vijijini uliibua hamasa miongoni mwa wana Chadema waliohudhuria mkutano ambao walimuunga mkono kwa kujichabhisha na kupatikana zaidi ya Sh300, 000 papo hapo.

Awali, Katibu wa Chadema jimbo la Sengerema, Paskazia Renatus ameueleza mkutano huo kuwa zaidi ya Sh350, 000 tayari zimechangwa kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja cha kujenga ofisi za chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live