Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amesema wao kama Chadema wapo tayari kukua mezani kufanya mdahalo na wapinzani wao, Chama cha Mapinduzi (CCM).
Amesema anaamini CCM hawana majibu ya hoja za Chadema kwani wao ndio walioifanya nchi iwe katika mahali ambapo ipo kutokana na uongozi wao.
"Sisi tupo tayari kufanya mdahalo na CCM kwa sababu wao ndio wana majibu ya haya mambo yanaendelea nchini, tunaamini kwamba siasa ni msuguano wa mawazo na mawazo bora ndio yachukue nafasi, tupo tayari jana kukutana nao, tupo zaidi ya tayari kufanya mahojiano lakini hiyo haituzuii kufanya maandamano akitaka kufanya mazungumzo na sisi amtafute katibu wetu Mrema hata leo jioni," alisema John Heche.