Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Heche: Polisi wameona madhara ya kukosa upinzani Bungeni

HECHE MSDKSD.jpeg John Heche

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime Mjini kupitia Chama cha Chadema, John Heche, amesema Askari Polisi wameona madhara ya kukosekana wabunge wa upinzani bungeni kwa kuwa wamekosa wasemaji wa changamoto zao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo tarehe 23 Januari 2023, Heche amedai kwamba kuna baadhi ya Polisi wamemfikisha malalamiko yao ambayo atayatoa kupitia mikutano hiyo.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo Polisi, hawatakubali chaguzi zijazo zichezewe.

“Kama walikuwa hawawezi kupambana na Chadema, leo Polisi wakiwa katikati wataweza kupambana? Sababu hata Polisi wameona madhara ya kukosa wabunge wa Chadema bungeni na wao wanalia na hoja zenu wameniletea nitazizungumza, kwa hiyo Polisi hawatakubali tena uchaguzi uibiwe sababu nao watakuwa kwenye moto,” amesema Heche.

Katika hatua nyingine, Heche ameitaka Serikali ihakikishe wananchi ambao ardhi zao zimechukuliwa kwa ajili ya uchimbaji madini, walipwe fidia.

By Mwandishi Wetu

John Heche

ALIYEKUWA Mbunge wa Tarime Mjini kupitia Chama cha Chadema, John Heche, amesema Askari Polisi wameona madhara ya kukosekana wabunge wa upinzani bungeni kwa kuwa wamekosa wasemaji wa changamoto zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo tarehe 23 Januari 2023, Heche amedai kwamba kuna baadhi ya Polisi wamemfikisha malalamiko yao ambayo atayatoa kupitia mikutano hiyo.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo Polisi, hawatakubali chaguzi zijazo zichezewe.

“Kama walikuwa hawawezi kupambana na Chadema, leo Polisi wakiwa katikati wataweza kupambana? Sababu hata Polisi wameona madhara ya kukosa wabunge wa Chadema bungeni na wao wanalia na hoja zenu wameniletea nitazizungumza, kwa hiyo Polisi hawatakubali tena uchaguzi uibiwe sababu nao watakuwa kwenye moto,” amesema Heche.

Katika hatua nyingine, Heche ameitaka Serikali ihakikishe wananchi ambao ardhi zao zimechukuliwa kwa ajili ya uchimbaji madini, walipwe fidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live