Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa Ndio Wagombea 9 Wanaowania Uspika wa Bunge - Video

DKT TULIA ACKSON Hawa Ndio Wagombea 9 Wanaowania Uspika wa Bunge - Video

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache ziliwa zimebaki kumfahamu atakayeongoza mhimili wa Bunge, Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema wagombea tisa watawania naafasi hiyo katika uchaguzi utaofanyika leo Februari 1, 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu uchaguzi huo na maandalizi ya uchaguzi Nenelwa amesema kuwa miongoni mwa Wagombea hao nane sio Wabunge na mmoja ni Mbunge.

Amewataja magombea hao kuwa ni;

1. Abdullah Mohammed Said (NRA)

2. Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP)

3. David Daud Mwaijojele (CCK)

4. Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA),

5. Kunje Ngombale Mwiru (SAU),

6. Maimuna Said Kassim (ADC)

7. Ndonge Said Ndonge (AAFP)

8. Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na

9. Dkt. Tulia Ackson (CCM)

Dkt. Tulia anapewa nafasi kubwa kushinda uchaguzi huo kutokana kwanza na uzoefu alioupata kwa miaka akiwa naibu spika, na chama chake kuwa na wabunge wengi. Baada ya uchaguzi huo, mchuano utahamia kwenye kumpata Naibu Spika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live