Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatushiriki Uchaguzi mdogo hadi Tume Uhuru ya Uchaguzi - CHADEMA

79664779 2837236583006984 4532831462549880832 N 660x400.jpeg John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifu Chama hakitashiriki Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ngorongoro na Kata 7.

CHADEMA imeitaka NEC kutotoa Fomu wala kufanya Uteuzi kwa yeyote atayetambulishwa kinyume cha Katiba ya Chama na barua kuwa ni Mgombea.

Imesisitiza kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi itakayohakikisha chaguzi zinakuwa Huru, za Haki na Halali kuanzia Uchaguzi wa marudio mpaka hadi Uchaguzi Mkuu.

Taarifa hii imetolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA taifa, John Myika na kusisitiza kuwa msimamo huo ni endelevu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live