Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Hatuoni tabu kuomba radhi kama tulitofautiana huko nyuma" - Kheri James

Screenshot 2021 03 29 At 03.17.47 660x400.png "Hatuoni tabu kuomba radhi kama tulitofautiana huko nyuma" - Kheri James

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa (UVCCM) Kheri James amesema UVCCM haioni tabu kuomba radhi kwa yeyote iwapo kuna mambo waliyafanya huko nyuma ambayo yalichochea chuki na uhasama na kuteteresha umoja na mshikamano wa Watanzania.

“Yawezekana katika siasa zetu na hekaheka zetu tuliweza kutofautiana kimitazamo, yapo mambo ambayo huko nyuma yalipelekea umoja wetu ukaterereka, UVCCM hatuoni aibu kusema tunaomba radhi kwa hayo kama tuliyatenda na tupo tayari kurekebisha ili kutengeneza jukwaa safi kwa Rais wetu kuanza upya akiwa na Watu walioshikamana na kuwa wamoja ili Nchi yetu iweze kwenda mbele”

“Sisi kama Vijana wa Mapinduzi kote Nchini tunao wajibu wa kushirikiana na Vijana wenzetu kuilinda dhamira hii ya Rais wetu ya kuwaleta Watanzania pamoja, kujenga mshikamano wao, kuzika tofauti zetu, ya kufungua kurasa mpya utakaotoa dira ya usawa, haki na maendeleo ya ukweli kwa Watanzania wote”

“Sisi Umoja wa Vijana CCM kamwe hatutokuwa kikwazo cha dhamira hiyo, kama kuna jambo huko nyuma ambalo kwa maneno au matendo ambalo linaweza kutumika kama rejea ya kuzuia hiyo dhamira ya Rais wetu sisi tunasema tunaomba radhi na tuko tayari kushirikiana na Rais wetu ili kuhakikisha dhamira yake haikwamishwi na matendo wala maneno yetu” – Kheri James.

FULL VIDEO: MWENYEKITI WA UVCCM KHERI JAMES AKIONGEA KUHUSU RAIS MPYA MHE. SULUHU NA KUHUSU ISHU YA KUOMBA RADHI.

Chanzo: millardayo.com