Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Tundu Lissu arejea Tanzania

Lissu Ef Hatimaye Tundu Lissu arejea Tanzania

Wed, 25 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amerejea rasmi nchini Tanzania leo Januari 25, 2023, akitokea nchini Ubelgiji alikokuwa uhamishoni.

Lissu amewasili katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika, John Heche, Peter Msigwa na viongozi waandamizi pamoja na wanachama na mashabiki wengine wa Chadema.

Aidha, msafara wake umeelekea viwanja vya Bulyaga uliopo Temeke Mwisho, ambapo utafanyika mkutano wa hadhara.

Lissu aliyekuwa Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema mwaka 2020, aliondoka nchini na kwenda Ujerumani kabla ya kwenda kuishi Ubelgiji tangu mwezi Novemba 2020, kwa kile alichodai kuwa usalama wa maisha yake uko hatarini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live