Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatima ya Lipumba CUF kujulikana leo

9d1abf5e396af63606fd385180df80c9 Profesa Ibrahim Lipumba.

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Ijumaa itatoa uamuzi wa kesi ya kuomba kumvua uongozi Mwenyekiti wa Chama cha Civic United Front (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Mussa Haji Kombo na mwanachama wa chama hicho, Juma Maimbo walifungua kesi hiyo wakiomba mahakama imvue uongozi Profesa Lipumba hadi kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mbali ya Profesa Lipumba, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Arubu Shamis, Naibu wake, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF. Kesi hiyo iko mbele ya Jaji Ephery Kisanya.

Kupitia Wakili Hashim Mziray, watoa maombi katika mawasilisho yao walidai kuwa waliwasilisha maombi hayo kutokana na uvunjifu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 toleo la mwaka 2014 ambalo limevunjwa na toleo la mwaka 2019.

Alidai mabadiliko yaliyofanywa na wadaiwa yameenda kinyume cha kilichoamuliwa na mkutano mkuu wa CUF wa mwaka 2019 kwani kuna baadhi ya vifungu havikupaswa kurekebishwa katika katiba hiyo.Mziray alidai kuna baadhi ha vifungu vimeongezwa katika toleo hilo la katiba ambavyo havikujadiliwa na mkutano mkuu na alikitaja kifungu hicho kuwa ni kinachohusu Kamati ya Itifaki na Udhibiti.

Alisema jambo hilo lililofanywa kwa uamuzi wa wadaiwa hao linahatarisha usajili wa chama kufutwa.

Wakili wa Profesa Lipumba, Mashaka Ngole na wenzake wakati akiwasilisha hoja za majibu kwa watoa maombi, pamoja na mambo mengine aliiomba mahakama kutokubali maombi hayo kwa sababu katika kiapo chao hawakuonesha namna gani katiba ya CUF imevunjwa na namna walivyoathirika.

Pia alidai katika kiapo hicho hawakuieleza mahakama wao ni kina nani wala uhusika wao katika chama hicho na hawakuonesha namna wadaiwa walivyofanya uvunjifu wa katiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live