Mwenyekiti wa Chma Cha Umma Hashim Rungwe amehudhuria katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kinachofanyika katika Ukumbi wa Mliamni City jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake fupi baada ya kupata nafasi Rungwe amedai anaunga mkono hoja ya vyama vya upinzani kuungana na kupaza sauti kwa pamoja kuhusu Katiba Mpya.
“Katiba tuliyonayo ni kwamba Rais hawezi kushtakiwa, sasa utamfanyaje katiba tuliyonayo inampa haki ya kuchagua kila mtu amtakaye, Halmashauri ile ya magomeni imejaa CCM watupu sasa we unategemea nini, Halmashauri zote nchini zimejaa viongozi wa CCM kwahiyo Katiba ndiyo mzizi wa fitina.” Alisema Rungwe.
Kwa upande mwingine mgeni mualikwa, mwanasiasa wa Chama cha Upinzania kutoka nchini Uganda Bobi Wine amesema kuwa ni Jambo jema kuwa na Katiba mpya na nzuri lakini kama kiongozi hataifuata na kuiheshimu itakuwa ni kazi bure.
Bobi ametolea mfano nchini kwake Uganda ambako amedai kuna katiba nzuri pengine nzuri kuliko Katiba zote Duniani lakini Kiongozi aliyeko madarakani hataki kuiheshimu katiba hiyo.
Baraza Kuu la Chadema kupitia mkutano wake huo linatarajiwa kutoa hatima ya wabunge wa viti maalum Chadema ambao waliingia Bungeni kupitia nafasi za kuteuliwa na aliyekuwa rais wa awamu ya Tano Hayati Rais John Pombe Magufuli.