Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamad Masoud ajivua uanachama ACT Wazalendo

Hamad Humud.jfif Hamad Masoud kabla ya kutimka ACT -Wazalendo

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekua Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa chama Cha ACT-Wazalendo Hamad Masoud Hamad ametangaza kujitoa na kuachia nafasi zote katika Chama Cha hicho.

Amesemea ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa Demokrasia katika chama.

"Nasema leo mimi Hamad Masoud Hamad si mjumbe tena wa Kamati Kuu na si Mwanachama tena wa ACT Wazalendo. Narudia tena kusema kama wao wanasema Hamad wa nini wako wanaosema watampata lini".

Katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa chama hicho Hamad Masoud alishindwa na Juma Duni Haji alishinda kwa kupata kura 339 sawa na asilimia 73.06 na Hamad Masoud alipata kura 125 sawa na asilimia 26.94

Hamad aliwahi kushika nafasi mbalimbali kupitia Chama Cha Wananchi, CUF na kuhudumu kama Mbunge wa Ole, visiwani Zanzibar kabla hajatimkia ACT-Wazalendo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live