Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri Kuu ya CCM Kukutana Desemba 18

Ccm Samia?fit=1000%2C667&ssl=1 Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu, kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kuanzia Desemba 15, 2021.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa vikao vyote ni vya kawaida kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live