Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halima Bulembo awataka vijana kutokata tamaa

68527 Bulembo+pic

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Halima Bulembo amedai alipojitosa kuwania nafasi hiyo alielezwa maneno ya kukatishwa tamaa lakini hakutaka kuyapa nafasi.

Akitoa salamu zake katika uzinduzi wa kampeni ya Kagera ya Kijani leo Jumamosi Julai 27, 2019 mbunge  huyo amewataka vijana kutovunjika moyo wanapogombea nafasi mbalimbali.

“Niliambiwa sina uwezo lakini mimi ni mbunge kupitia vijana mkoani Kagera,” amesema Halima na kuwataka vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

Katika uzinduzi huo, Joyce Robozi ametambulishwa kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la walimu makada wa CCM na kuahidi kulinda mafanikio ya Serikali.

Uzinduzi wa Kagera ya kijani umetajwa kuwa ni mkakati kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba, 2019.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz