Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna nchi isiyokopa-UVCCM

Uvccm Pic Data Hakuna nchi isiyokopa

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa umoja wa vijana Taifa (UVCCM), Kenan Kihongosi amesema duniani kote hakuna nchi isiyokopa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya jipya.

Kihongosi amesema hayo leo Desemba 31, 2021 wakati akikagua mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kihesa mkoani Iringa.

Amesema hata wabunge wanachukua mikopo mikubwa hivyo suala la nchi kukopa fedha kwao sio hoja isipokuwa faida zake.

“Ndani ya siku chache kumekuwa na matamko yasiyoeleweka kuna baadhi ya viongozi wanakosoa na kuona kwamba mikopo hii haina tija, tangu awamu ya kwanza mpaka sasa hakuna awamu ambayo haikukopa fedha kwanini haya makelele yaanze baada ya awamu ya 6 kuwa madarakani,” amesema Kenan

Amesema Serikali ya awamu ya 6 imekopa fedha ndogo zaidi kuliko fedha zote zilizowahi kukopwa tangu nchi ipate uhuru.

“Deni letu linakalibia tirioni 70, Rais Samia Suluhu amekopa tirion 1.3 tu na fedha hiyo ameiweka wazi Watanzania mnajua inaenda kufanya shuguli gani madarasa nchi nzima yamejengwa na wanufaika wakubwa ni watoto wa Watanzania masikini”

Kihongosi amesema kuwa mwaka uliopita wazazi walikuwa wakichangishwa michango ya kujenga madarasa na kuna watu walikuwa wanakimbia familia zao ili waweze kukwepa michango.

“Wito wangu viongozi ambao wanazungumza katika mitandao na vyombo vya habari watambue kuwa Watanzania tunajua nini Rais wetu anafanya lakini lazima pia watambue dunia inatambua nini Rais Samia anafanya ndani nan je ya nchi wanamjua Raisi wetu anafanya kazi gani kwa taifa”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live