Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna maadili, vijana wanatujana - Ally Hapi

Hapi WA0007 Ally Hapi

Sat, 4 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Ally Hapi amewataka Wazazi kuungana kuhakikisha kunakuwa na maadili mema katika Jamii ili kuondoa tabia zisizofaa ikiwemo za Vijana wanaotukana mitandaoni.

Akiongea leo May 04,2024 akiwa kwenye ziara yake Mufindi Mkoani Iringa, Hapi amesema “Tunafika mahali tunakuwa na Jamii ambayo haina maadili, sisi kama Jumuiya ya Wazazi wajibu wetu ni kuhakikisha kunakuwa na maadili mema kwenye Jamii, tufanye makongamano na semina za kuelimisha Wazazi, tutoe elimu kupitia Radio juu ya namna gani ya kulinda maadili mema.”

“Leo Vijana wanatukana tu mtandaoni na inaonekana ni utaratibu wa kawaida jambo ambalo lilikuwa aibu kipindi cha nyuma, kuna dhana potofu kwamba Jumuiya ya Wazazi ni ya Wazee au Wastaafu sasa unaona Mwenyekiti wetu ni Kijana, huu uvumi unaoenea hauna lengo zuri la Jumuiya za Wazazi una lengo la kuwakimbiza Vijana na akina Mama.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live