Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HIZI NDIO AHADI ZA JPM KWA WATANZANIA

Image 455.png?fit=591%2C312 HIZI NDIO AHADI ZA JPM KWA WATANZANIA

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

“Miaka mitano ya uongozi wangu tumefanikiwa kujenga hospitali ya wilaya ya Bahi mbayo hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 95” – Mgombea urais CCM, Rais John Magufuli

“Nataka miaka mitano ijayo watoto katika Wilaya ya Bahi waendelee kusoma bure, masuala la kufukuzwa ada na michango sitaki kuisikia”– Mgombea urais CCM, Rais John Magufuli

“Miaka mitano ijayo nitahakikisha vijiji 16 vya Wilaya ya Bahi ambavyo havijafikiwa na huduma ya umeme viwe vimefikiwa”– Mgombea urais CCM, Rais John Magufuli

“Miaka mitano ijayo nitahakikisha wananchi wa Wilaya ya Bahi wanapata huduma ya afya, tutajenga shule, madarasa sambamba na kuongeza idadi ya walimu”– Mgombea urais CCM, Rais John Magufuli

“Kero ya huduma ya maji katika Wilaya ya Bahi inaniumiza sana, miaka mitano ijayo nitahakikisha shida hiyo inamalizika. Sasa hivi tumeanza na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa mradi wa maji wa Ibimwa, ninawahakikishia kero ya maji itabaki historia” – Mgombea urais CCM, Rais John Magufuli

“Miaka mitano yangu ya utawala ilikuwa ninawaonjesha tu, Sasa miaka mitano ijayo ndiyo itakuwa yenyewe katika uchapaji kazi”– Mgombea urais CCM, Rais John Magufuli

Chanzo: zanzibar24.co.tz