Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima adai taarifa zaidi kuhusu chanjo ya Uviko-19

11cf2165eddbda572ab326828de9dc4c Gwajima adai taarifa zaidi kuhusu chanjo ya Uviko-19

Sun, 5 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima amesema yeye na Baraza la Maaskofu wa kanisa lake hawajapata taarifa za kutosha dhidi ya madhara ya chanjo ya UVIKO-19 katika kipindi cha muda mfupi, siku zijazo na miaka mingi ijayo.

Gwajima amesema hayo leo wakati akiendesha ibada katika kanisa lake na kwamba hayo ni miongoni mwa sababu kuu ya yeye na baraza hilo kutojihusisha na chanjo ya UVIKO-19 inayoendelea kutolewa nchini.

Hata hivyo wataalamu wa afya wameeleza mara kadhaa kwamba kupata athari mbaya baada ya kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19 ni kawaida na inaweza kuwa ishara kwamba chanjo inafanya kazi.

Wataalamu wanadai baada ya chanjo, mtu anaweza pata homa, maumivu, au uchovu. Kutegemea na binadamu, kila mtu anaweza kupata moja ya dalili hizo, ama zote kwa wakati mmoja au kutoona dalili zozote. Athari hizi zinaweza kuonekana na kuondoka kati ya saa hadi siku kadhaa.

Gwajima ameeleza kuwa baada ya kuitwa na Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge alitakiwa ajitete lakini alisisitiza kuwa hajapata taarifa za kina.

“Nilikuwa very straight (moja kwa moja) na nikawaambia nataka nikifanye kikao hiki kiwe kifupi. Askofu wa kanisa amezungumza kanisani kwake akiongea na wanaumini wake. Na kwamaana hiyo nilikua nazungumza na watu wangu.

“Nilisema straight wala sikupindisha chanjo ni hiari. hatahivyo Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wanahitaji taarifa ya kutosha juu ya madhara ya muda mfupi, siku zijazo na madhara ya miaka mingi kuhusu chanjo ya UVIKO-19”alisema Gwajima.

Alisisitiza “mpaka sasa hivi hatujapata taarifa. Na huo ndio ukorofi wangu. Kamati ya Bunge waliomba nijitetee nikasema sina cha kujitetea kwa kuwa mahubili yanatoka kwa roho mtakatifu.”

Chanzo: www.habarileo.co.tz