Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima: Wengi Wapo Mahabusu Wamebambikiziwa Kesi za Uhujumu Uchumi

Gwajima?fit=800%2C453&ssl=1 Gwajima: Wengi Wapo Mahabusu Wamebambikiziwa Kesi za Uhujumu Uchumi

Fri, 23 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mchungaji Dkt. Josephat Gwajima, amesema, kuna idadi kubwa ya watu wako mahabusu kutokana na suala la utakatishaji wa fedha ambao wako waliobambikiziwa kosa hilo na watumishi wasio waaminifu wa vyombo vya dola na kuomba suala hilo liangaliwe kwa kina.

Gwajima amesema hayo leo Ijumaa, Aprili 23, 2021, Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.

“Mpaka leo kwa mujibu wa takwimu kuna watu 1,701 ambao wako mahabusu kwa sababu ya ama kwa ajili ya utakatishaji fedha Money laundering au kwa sababu ya uhujumu uchumi.

“Unakuta mtu anakwenda kwa mfanyabiashara kukusanya mapato au kudai mapato au malimbikizo ya mapato anakwenda na ‘charge’ kabisa kwamba usiponipa fedha kadhaa tayari nina hati hii hapa nakuwekea Money laundering au nakuwekea Economic Sabotage.

“Kuna watu wengi sana Naibu Spika wako ndani, wako mahabusu maelfu ya watu kwa sababu ya hili suala la utakatishaji fedha kubambikiziwa na watu wasio waaminifu katika vyombo vyetu vya Dola”.Gwajima,” Mchungaji Dkt. Josephat Gwajima.

Chanzo: globalpublishers.co.tz