Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Freeman Mbowe kizambani kesho

Freeman Mbowe Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania.

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Jeshi la Polisi kumkamata na kumhusisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na tuhuma za mauaji na makosa ya ugaidi, kesho siku ya Alhamisi atafikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka hayo.

Mbowe na baadhi ya viongozi wa Chadema walikamatwa Julai 21 jijini Mwanza wakati wakijipanga kufanya kongamano la Katiba lililopigwa marufuku jijini humo.

Hata hivyo, Mbowe alisafirishwa kutoka Mwanza kuja Dar es Salaam ambako alipekuliwa nyumbani kwake, huku taarifa iliyotolewa na Polisi juzi ikieleza kuwa Mbowe alikamatwa akihusishwa na makosa ya ugaidi na njama za kutaka kuua viongozi wa Serikali.

Polisi nchini Tanzania imesisitiza kuwa Mbowe amefanya makosa na ushahidi upo.

‘’Wafuasi wa CHADEMA wanadhani Mbowe ameonewa na kuwa yeye ni malaika hawezi kufanya makosa, lakini kesi hii iko mahakami hivyo tuachie mahakama ifanye kazi yake na ukweli utajulikana’’ alisema IGP Simon Sirro mkuu wa polisi Tanzania mapema wiki hii.

Mbowe alikamatwa wiki mbili zilizopita na baadae kusomewa mashtaka ikiwemo ugaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live