Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fred Vunjabei ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya fedha, Uchumi UVCCM

02902368 3100 43ef B890 1d1981495db9 Mfanyabiashara Fred Ngajilo "Vunja Bei"

Tue, 25 May 2021 Chanzo: mtanzania.co.tz

Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu ‘Fred Vunja bei’ amepitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha Taifa.

Fred amepitishwa kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la Mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio.

Aidha, mbali na Fred, Umoja huo umempitisha, Rose Manumba kuwa Katibu wa idara hiyo. Baraza hilo lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na visiwani.

Chanzo: mtanzania.co.tz