Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fred Vunja Bei, Babu Tale waula UVCCM

Db895aa285c6c6e5ce32833316c0d5a6.jpeg Mfanyabiashara Fred Ngajilo "Vunja Bei"

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(UVCCM) limemteua Fred Ngajiro ‘Vunja Bei na Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’ kuongoza kamati ndogo ya Uchumi, Fedha na Uwezeshaji ndani ya Jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa UVCCM, Raymond Mwangwala alisema katika kikao cha kamati hiyo kimeunda kamati ndogo ya Uchumi, Fedha na Uwezesheshaji ikiongozwa na Fred Ngajiro maarufu kama ‘Fred Vunja Bei’ (Mwenyekiti) na Rose Manumba (Katibu) huku wajumbe wakiwa ni Hamis Taletale ‘Babu Tale’, Tofiq Turky na Gwanta Alex.

Kamati hiyo ina jukumu la kuhakikisha wanashauri na kusimamia vitega uchumi yote vya umoja huo

Pia Baraza kuu limemvua uongozi Hussen Salehe aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya ya moshi vijijini kwa kutokuwa na maadili pamoja na nidhamu baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa wa Kilimanjaro.

"Baraza Kuu lilijiridhisha, Kamati ilijiridhisha na kuona kwamba kwa tuhuma zile na mapendekezo yaliyotolewa katika kikao Halmashauri Kuu ya mkoa hivo limemvua uongozi.

“Hivyo naagiza mkoa wa Kilimanjaro kutangaza nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM, katika wilaya ya Moshi Vijijini”alisema.

Sambamba na hayo UVCCM pia imeazimia kumuenzi hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kwa kuyaendeleza yale yote mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uhai wake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz