Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fred Lowassa ampeleka Mkumbo Monduli kwenye mradi wa Bilioni 396 (+picha)

WhatsApp Image 2021 08 14 At 00.13.57 5 660x400.jpeg Fred Lowassa ampeleka Mkumbo Monduli kwenye mradi wa Bilioni 396 (+picha)

Sat, 14 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amaeeleza kuwa Serikali ipo mbioni kuanza utekelezaji wa Mradi wa Magadi Soda katika Bonde la Engaruka Wilaya ya Monduli mkoani Arusha ambao ni moja kati ya miradi 17 ya kimkakati katika kujenga uchumi wa viwanda nchini kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDPIII) 2021/2022 – 2025/2026.

Prof. Mkumbo ameeleza hayo Agosti 13, 2021 wakati alipoambatana na Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa kutembelea eneo ambalo mradi huo utatekelezwa liliopo kilomita 190 Kaskazini Magharibi mwa Jiji la Arusha katika Wilaya ya Monduli ambao utekelezaji wake utawezesha ukuaji wa viwanda na uzalishaji wa fursa za ajira.

“Mradi huu wa Magadi Soda ni mradi mkubwa na muhimu sana ndio maana Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeuingiza katika miradi kumi na saba nchi nzima ya kielelezo kwenye Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ambayo inabeba uchumi wa nchi katika kipindi cha miaka mitano” Prof. Kitila Mkumbo

Mradi huo unasimamiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo na sasa hatua ya upembuzi yakinifu imekamilika na imeonesha uwepo wa takriban mita za ujazo 3,294,704,894 za magadi hivyo uzalishaji huu utaweza kukidhi mahitaji ya ndani ya nchi, ukanda wa Afrika Mashariki na soko la kimataifa na utatoa ajira kwa watu wasiopungua 500.

Aidha, Prof. Mkumbo amaeeleza kuwa hatua iliyopo kwa sasa ni kutafuta mwekezaji atakayeshirikiana na Serikali kutekeleza mradi huo na magadi yatakapopatikana yatakuwa malighafi katika mambo mengi kama Kutengenezea vioo vya aina zote, Kutengenezea sabuni, karatasi, Kusafisha maji, Kusafishia madini, Kupunguza athari za gesi yenye sumu zinazotoka viwandani na sehemu nyingine nyingi.

Prof. Mkumbo amewatoa hofu wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya mradi kuwa kabla ya mradi huo kutekelezwa mwananchi watapewa elimu kuhusu huo mradi na kila mmoja atalipwa fidia kulingana na tathimini iliyofanyika kwa wananchi wote 599 na ndio mradi utaanza kutekelezwa.

Nae, Mbunge wa Monduli Fredrick Lowassa ameipongeza Serikali na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mradi huo kwenye miradi ya kimkakati ambao ndani ya miaka mitano lazima ikamilike na ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kusimamia na kukamilisha suala la fidia kwa wananchi wakati huo akieleza manufaa na jinsi wananchi wa Monduli watakavyofaidika na mradi huo wa magadi soda.













Chanzo: millardayo.com