Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fred Lowassa afanya ziara Monduli, achangia zaidi ya Milioni 6 (+picha)

Screenshot 2021 05 03 At 10.49.55 660x400.png Fred Lowassa afanya ziara Monduli, achangia zaidi ya Milioni 6 (+picha)

Mon, 3 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Monduli  Fredrick Edwad Lowassa. akiambatana na Mkuruagenzi wa ECLACT Foundation Peter Toima pamoja na Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Monduli alitembelea kijiji cha Indonyoonado.

Katika ziara hiyo alianza kwa kukagua eneo  litakalo jengwa Nyumba ya Daktari ambayo Mbunge Fredrick Lowassa kupitia mfuko wa Jimbo amechangia  Shilingi Milioni 6,805,755.

Baada ya hapo Lowassa akiambatana na Mkurugenzi wa ECLAT alitembelea eneo la Shule ya Msingi ya Indonyonado na kujionea Jengo lililoezuliwa na upepo ambalo limejengwa kwa nguvu za Wananchi.

Aidha Mbunge Lowassa baada ya kukagua miradi hiyo alizungumza na Wananchi waliojitokeza kumpokea.

Akizungumza na Wananchi hao Fredrick alianza kwa kuwashukuru wananchi  wa kijiji hicho kwa kumchagua kwa kura nyingi yeye pamoja na aliekuwa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa 93%.

Pamoja na shukurani hizo Lowassa alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi hao kuwa baada ya kutokea msiba Mkubwa wa kitaifa na kumpoteza aliekuwa Rais  wa awamu ya tano,  sasa tunaye  Rais  Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani.

Lowassa alitumia nafasi hiyo kumtambulisha na kumkaribisha Mkurugenzi wa ECLAT Foundation kwa kusaidia Wilaya ya Monduli kwa kupitia Shirika hilo.

Lowassa alimweleza Mkurugenzi huyo wa ECLAT kuwa yeye baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge, Kipaumbele chake ni Elimu Elimu Elimu hivyo alimuomba mfadhili huyo kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na Ofisi ya Mkurugenzi kusaidia kujenga Shule ya Msingi Endonyonaado ambacho wananchi walijenga  madarasa mawili na kupauwa lakini  upepo uliezua. 

Baada ya hapo Mbunge alimkaribisha Mkurugenzi huyo  wa shirika la ECLAT DC mtaafu  Peter Toima. 

Akizungumza na adhara hiyo Peter Toima alimshukuru Lowassa kwa kumkaribisha katika Wilaya ya Monduli na kumleta Kijiji cha Indonyonaado na Toima aliwaeleza wananchi hao kuwa Mbunge  wa Jimbo la Monduli alitembelea  Makao Makuu ya Shirika la ECLAT  Wilayani Simanjiro na ndipo alipo nipa mwaliko wa kuja kutembelea Kata ya Mfereji.

Kwa heshima hiyo na umuhimu wake alionionyesha Mbunge wa Jimbo la Monduli ninamuahidi kumuunga mkono wa dhati,  Mbunge naomba nikajiandae kwa kazi hiyo na niaahidi mwezi wa saba ikimpendeza Mwenyenzi Mungu nakuja na wafadhili eneo hili la Indonyonaado. 

Baada ya hapo Mbunge Fredrick Lowassa na msafara wake walitembelea Zahanati  Kata ya Engutoto Kijiji cha Mlimani na alipata nafasi ya kuongea na Serikali ya Kijiji cha Mlimani na kueleza kwamba kupitia Mfuko wa Jimbo amewapa Million tano.

Na baada ya hapo Mbunge alimkaribisha Mkurugenzi wa ECLAT ambaye ni mgeni wake kwenye Kijiji cha Mlimani naye kwa furaha na kwa kuona juhudi za Mbunge akamuunga Mkono kwa Shilingi Million tano. 

MEI MOSI: “TULIKUJA NA MATARAJIO YAKUONGEZWA, HATA KWA PUNGUZO TUNASHUKURU”

Chanzo: millardayo.com