Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fred Lowassa: Tumerejea nyumbani CCM

45786 Lowassapic Fred Lowassa: Tumerejea nyumbani CCM

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mamia ya wakazi wa Arusha wamekusanyika uwanja mdogo wa Arusha kumsubiri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa aliyetimkia Chadema akitokea CCM ambako alipitishwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Mei mosi, 2019 alitangaza kurudi CCM na leo Jumamosi Mei 9, 2019 anarejea nyumbani kwake, Monduli mkoani Arusha.

Watu hao wakiwepo familia ya Lowassa, wakiongozwa na mtoto wake, Fred Lowassa wamesema wamerejea nyumbani CCM na Lowassa.

Fred ambaye naye alijiunga na Chadema baada ya baba yake kutimkia Chadema Julai 28, 2015, amesema familia yote ya Lowassa imerejea nyumbani CCM.

"Kama alivyosema mzee amerudi nyumbani na sisi kama familia tumerudi kumuunga mkono" amesema Fred leo Jumamosi Machi 9, 2019 jijini Arusha.

Amesema anajisikia vizuri kurudi nyumbani kuendelea kushirikiana na rafiki zake ambao aliwaacha CCM na ambao bado wapo Chadema.

Soma Zaidi: Aliyofanya Edward Lowassa Chadema ndani ya siku 1,312

Baadhi ya makada wa CCM, walieleza Lowassa amefanya jambo zuri kurejea CCM kwani ndicho chama alichokulia.

Jeremiah Peter na Wilbard Shoo wanampongeza Lowassa kurejea nyumbani CCM.

Soma Zaidi: Sasa ni Lowassa vs Chadema

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendea



Chanzo: mwananchi.co.tz