Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fedha za vyoo majimboni kaa la moto bungeni

63429 Pic+vyoo

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Fedha za ujenzi wa vyoo vya mfano kwa wabunge majimboni nchini Tanzania zinaendelea kuligawa Bunge huku baadhi wakitilia mashaka ziko wapi na kiasi gani.

Leo Jumatano Juni 19,2019 wabunge wa CCM Ally Keissy (Nkasi) na Mwita Getele (Bunda) wamehoji juu ya fedha hizo ambazo zilichangishwa na wabunge wanawake kwa njia ya harambee, matembezi na michango ya wabunge na wahisani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Keissy aliomba mwongozo akihoji fedha hizo ziko wapi, zinafanya nini na kwa nini wabunge wasirudishiwe michango yao.

Jana, Spika wa Bunge, Job Ndugai alitoa ufafanuzi kuwa fedha hizo ziko katika mikono salama na kwamba unafanyika utaratibu mzuri wa utekelezaji wake huku akibainisha zikiingizwa akaunti za wabunge kuna baadhi wanadaiwa na mabenki zitakatwa.

Leo wabunge hao wamezidai tena huku Keissy akitaka Bunge kuwa mfano kwani kukaa kimya wakati Serikali inasisitiza uwazi si jambo jema.

Naibu Spika Dk Tulia Akson amesema fedha hizo ziko ofisi ya uhasibu bungeni na kutaka wabunge kuondoa mashaka kwani watasababisha walioahidi wasitoe.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz