Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya Mwalimu Nyerere yaja kivingine

Mwalim Makamu Mwenyekiti wa familia ya Mwalimu, Dkt Joachim Nyerere akifafanua.

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya Muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wanatarajia kuandaa Tamasha "Jukanye Festival" kutimiza miaka 100 ya kuzaliwa kwake.

Tamasha hilo litafanyika Aprili 20 mwaka huu Butiama Mkoa w Mara , Musoma kwa lengo la kumuenzi na kushiriki burudani mbalimbali.

Makamo Mwenyekiti wa familia hiyo Dk. Joachim Nyerere amesema Tamasha Hilo litakuwa la siku tatu ambapo kilele kitafanyika Aprili 20 mwaka huu

"Mwalimu Julius Nyerere alizaliwa Aprili 13 siku hiyo itakuwa ibada kwa ajili ya kumuomba Mungu, hivyo tumesogeza mbele hadi Aprili 20," amesema.

Dk. Joachim alieleza kuwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa mpenzi wa muziki siku hiyo kutakuwa na Matukio mbalimbali ya burudani.

"Mwalimu Nyerere alikuwa mdau kubwa wa burudani siku hiyo kutakuwa na Matukio tofauti ya burudani ambayo yatapamba tamasha hilo ".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live