Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu zigo linalomkabili Silaa Wizara ya Ardhi

Sd Silaaa Fahamu zigo linalomkabili Silaa Wizara ya Ardhi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo kumiliki ardhi na watumishi wa ardhi kuwa na maslahi katika upimaji, ni miongoni mwa mambo magumu yatakayomkabili Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

Kwa mujibu wa wabunge, ugumu wa wizara hiyo unakuja pale ambapo maeneo nyeti nchini yanamilikiwa na wale waliowaita vigogo, hivyo inahitaji moyo wa chuma kuwashughulikia.

Kauli za wabunge kuhusu ugumu huo, zinakuja wiki moja tangu mbunge huyo wa Ukonga jijini Dar es Salaam, aapishwe kushika wadhifa huo ambao awali ulikuwa chini ya Dk Angeline Mabula aliyekuwa akikabiliwa na rundo la migogoro ya ardhi. Kwa mujibu wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/24 iliyowasilishwa na mtanguzi wake, Mabula inaonyesha hadi kufikia Mei 15 mwaka huu migogoro 2,684 ilikuwa imeshughulikiwa kiutawala.

Jijini Dodoma, migogoro 815 ilipokelewa ambapo 429 sawa na asilimia 52.6 ilipatiwa ufumbuzi na 386 inaendelea kushughulikiwa huku Mkoa wa Dar es Salaam, migogoro 386 ilipokelewa, 201 sawa na asilimia 52 ilipatiwa ufumbuzi na 186 iliyosalia inaendelea kupatiwa ufumbuzi.

Tangu alipoapishwa, Silaa ameonekana mara kadhaa kuzungumza na menejimenti ya wizara hiyo na msisitizo wake ni kuomba ushirikiano na kuwataka watumishi wake kumaliza migogoro ya ardhi ndani ya siku 100 na kula sahani moja na wazembe.

Pamoja na mwanzo wa ahadi na msisitizo wa utendaji, inamhitaji moyo wa chuma kwa kuwa nafasi yake hiyo ya kushughulika na ardhi si jambo lelemama, kama anavyoelezwa na wabunge wenzake walipozungumza na gazeti hili.

Mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara alisema inahitaji moyo kuwasaidia wananchi wa ngazi ya chini, ilhali maeneo nyeti ya ardhi yanamilikiwa na vigogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live