Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duni awataka ACT -Wazalendo kushikamana

Duni Pic Data Juma Haji Duni, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo wamehimizwa kudumisha umoja, mshikamano na upendo miongoni mwao ili chama hicho kupata mafanikio.

Ushauri huyo  umetolewa na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa,  Juma Duni  Haji wakati alipokuwa anazungumza kwenye kikao cha ndani  na wanachama  wa ACT Mkoa wa Lindi kilichofanyika  ukumbi wa MM Hotel.

Duni amesema ili chama kiweze kufikia malengo wanachama hawabudi kujenga umoja na mshikamano na  endapo wana ACT-Wazalendo hawatashikamana katika ujenzi na uimarishaji wa chama chao ipo hatari ya mamluki kuingia miongoni mwao, na kuwavuruga kwa lengo la  kuharibu umoja na,mshikamano wao.

Amesema kuwa uongozi wa chama umejipanga kuhakikisha chama kina imarika, lakini hayo hayataweza kukamilika kama wanachama hawatakuwa na moyo wa umoja na mshikamano

"Uongozi umejipanga  kujenga chama na kupiga kelele kupata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya hivyo wanachama wana wajibu wa kujenga umoja na mshikamano" amesema Duni

Amewataka wanachama wa ACT-Wazalendo kujiunga uanachama kwa njia ya kidigitali ili kurahisisha ukusanyaji mapato na utoaji huduma ikiwemo uhakiki wa wanachama.

Advertisement Kwa upande wake mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Kanda ya Kusini, Selemani Bungara amesema kuwa     kanda ya kusini wako imara wanajipanga kuhakikisha chama kinasonga mbele.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz