Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duni aeleza alichoteta na Rais Samia, Dk Mwinyi

Duni Act Act Duni aeleza alichoteta na Rais Samia, Dk Mwinyi

Sat, 18 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji amesema Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Mwinyi wanapaswa kukumbuka umuhimu wa Katiba Mpya kwa kuwa Tanzania inahitaji mchakato huo uanze hivi sasa.

Pia, katika mazungumzo yake na viongozi hao, Duni maarufu Babu Duni amewaambia kuhusu kupatikana tume huru ya uchaguzi itayosimamia kura ya maoni ya Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa Duni, alifikisha ujumbe alipokutana na viongozi hao wakuu wa Tanzania na Zanzibar kwa nyakati tofauti akianza na Dk Mwinyi aliyekutana naye Aprili 25,2022 kisha akaonana na Rais Samia Mei 5,2022.

Mbali na hao, Duni alikutana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume. Hata hivyo, licha ya kukutana na viongozi hao, mazungumzo yao hayakuwekwa wazi.

Lakini leo Jumamosi Juni 18, 2022 katika kongamano la tatu la ACT-Wazalendo kuhusu tume huru ya uchaguzi, Duni ameeleza masuala mbalimbali alioteta likiwemo la Katiba Mpya baada ya kukutana na viongozi hao. Kongamano lilifanyika Songea mkoani Ruvuma likishirikisha wanachama na viongozi mbalimbali wa ACT-Wazalendo.

Duni amesema katika mazungumzo yake na Rais Samia pamoja na viongozi wengine, aliwasisitiza hoja  ya ACT-Wazalendo kwamba Tanzania inahitaji Katiba Mpya na kwamba haitaishia kwa viongozi hao bali ataonana na viongozi wa CCM na vyama vingine.

Advertisement Hata hivyo, Duni amesema kumekuwa na dalili za njema za Taifa kuongozwa kwa kufuata misingi na taratibu zilizowekwa, akimpongeza Rais Samia kwa kuonyesha uthubutu katika masuala mbalimbali yanayoashiria umoja na mshikamano wa nchi.

Amebainisha kuwa katika kuelekea hatua hiyo, kunahitaji pia mabadiliko mbalimbali katika kipindi cha mpito ikiwemo kuzifanyia marekebisho sheria za uchaguzi, Katiba Mpya na kura ya maoni.

"Ni lazima tupate Katiba Mpya itayoendana na mazingira ya demokrasia ya vyama vingi badala ya Katiba ya sasa iliyotungwa wakati wa chama kimoja. Pia kuna haya kuwa Tume Huru ya Uchaguzi," amesema Duni.

Duni amesema mambo mengine aliyoteta na viongozi hao ni kuhusu maridhiano ya kisiasa na muafaka wa kitaifa, kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini na kuchukua hatua za dharura za kuwakwamua Watanzania kiuchumi.

Makamu mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, Dorothy Semu amesema Ruvuma ni miongoni mwa mikoa ya kilimo, hivyo chama hicho kitahakikisha kinawapigania wakulima katika masuala mbalimbali ikiwemo bei nzuri ya mbolea ili kuleta unafuu kwa kundi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live