Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duni Haji afichua jinsi walivyomshawishi Karume kuendelea kuongoza

Duni Haji Tena Duni Haji afichua jinsi walivyomshawishi Karume kuendelea kuongoza

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kada wa Chama cha ACT-Wazalendo na mwanasiasa mkongwe visiwani Zanzibar ,Juma Duni Haji amefichua jinsi ambavyo mwaka 2009 walimshawishi aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo, Aman Karume abadili Katiba ili aendelee kuongoza baada ya kumaliza kipindi cha miaka 10 kwa kuwa alionesha nia njema.

Alisema tofauti na wana CCM wengine Rais Karume na Maalim Seif walikuwa wameamua kwa dhati kuzika tofauti za kisiasa katika visiwa hivyo na kuachana na siasa zilizowagawa Wazanzibari.Duni akizungumza katika maadhimisho ya hayati Maalim Seif jana alisema mbegu alizozipanda kiongozi huyo zitaendelea kumea na kwamba kwa sasa wanaendelea kuzungumza na Rais Hussein Mwinyi ili yasitokee machafuko wala mivutano tena kipindi cha uchaguzi.

Kada huyo ambaye ameshatangaza nia ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa chama chake alisema kwamba kutokana na mazoea yaliyokuwepo Maalim Seif alikuwa ndiye alama ya chama na ukombozi wa wananchi na kuondoka kwake ghafla kulileta mfadhaiko kwa wanachama lakini kwa sasa lazima harakati ziendelee.

"Tuliathirika sana na kuondoka kwake kwasababu tulijenga mazoea akawa yeye kama ndiyo 'Icon' ukitaja ACT- Wazalendo maana yake unamtaja Maalim Seif unaona yeye ndiyo mkombozi sasa ile ghafla hayupo watu waliona sasa mwokozi wetu kaondoka, sisi tunachoamini ametutayarisha vijana wengi sana katika chama ambao sasa tunaweza kuchukua nafasi yake na kuendeleza harakati zile alizoziacha na nina hakika mambo yatakwenda.

Sisi baada ya miezi miwili mitatu tutakuwa na uchaguzi wa Mwenyekiti, tukishapata Mwenyekiti wa chama harakati zitaonekana tena za kushusha tanga na kupandisha tanga na kuhusu maridhiano Mheshimiwa Othman anaendelea kuzungumza na Rais ili yale yaliyotokea 2020 yasitokee tena."-Juma Duni Haji

Chanzo: ippmedia.com