Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr. Tulia aingia kwenye mifereji ya maji machafu kusafisha (+picha)

WhatsApp Image 2020 12 18 At 12.55.35 660x400.jpeg Dr. Tulia aingia kwenye mifereji ya maji machafu kusafisha (+picha)

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

December 18, 2020 Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ameungana na Wananchi wa maeneo mbalimbali kwa lengo la kufanya usafi katika mfereji wa maji wa Ilolo unaokusanya maji kutoka katika kata saba za Jiji la Mbeya.

“Siku ya Jumatatu nilikuja kukagua hii mifereji baada ya kuelezwa kuhusu changamoto wanazopitia Wananchi kwa hii mifereji pindi inapoziba na kusababisha maji kuingia kwenye nyumba za watu na nikapendekeza itapofika siku ya leo wote tuungane kwa lengo la kufanya usafi kila eneo la mifereji na niwashukuru sana kwa muitikio wenu mkubwa”-Dr. Tulia Ackson

“Naamini zoezi hili likiwa endelevu itatusaidia kupunguza kasi ya mafuriko ambayo yamekuwa yakitukumba mara kwa mara hususani katika vipindi vya mvua ambayo zaidi yamekuwa yakitokana na kuzibwa kwa hii mifereji, tujitahidi pia kuwa wasafi na tuache tabia za kutupa takataka katika mitaro”-Dr. Tulia Ackson

HAYA NDIO MAAGIZO YA NDALICHAKO KWA MA-RC, DC

Chanzo: millardayo.com