Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr. Stagomena ameapishwa rasmi kuwa Mbunge

Taxdrtax Mbunge Dr.Stregomena Tax

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa kuteuliwa,Dr.Stregomeena Tax ameapishwa muda mfupi leo Bungeni Dodoma baada ya Rais Samia kumteua kuwa Mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge huyo anajaza nafasi 10 za Wabunge wa kuteuliwa na Rais, na hapo awali kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Katibu Mtendaji wa SADC na amemaliza muda wake mwezi August mwaka 2021.

Aidha Muundo wa Bunge la Tanzania una makundi matano amabayo yameanishwa katika Ibara ya 6 ya katiba ya Tanzania, ambapo kuna Wabunge wa kuchaguliwa na wananchi ambao huwa ni 239, Wabunge wa viti Maalumu huwa ni 102, Wabunge wa uwakilishi kutoka Zanzibar 5, na Mwanasheria Mkuu nafasi 1, na wabunge wa kuteuliwa na Rais nafasi 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live