Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dorothy Semu atafakari kumrithi Zitto Kabwe

Dorothy Kumrithi Zitto Dorothy Semu atafakari kumrithi Zitto Kabwe

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: Mwananchi

Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Tanzania Bara, Dorothy Semu amesema anatafakari juu ya kugombea nafasi ya Kiongozi wa chama hicho na kwamba kipenga kikipulizwa watamuona kwenye kinyang’anyiro.

Dorothy amesema hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi Januari 3, 2024 alipozungumzia masuala mbalimbali ya kiuongozi ndani ya chama chake na maisha yake binafsi.

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe anatarajiwa kumaliza muda wake Machi 29, 2024, hivyo utafanyika uchaguzi wa kutafuta mrithi wa kiti hicho na tayari watu sita wanatajwa kuwania nafasi hiyo akiwamo Dorothy, Ismail Jussa, Othman Masoud Othman, Issihaka Mchinjita, Emmanuel Mvula na Ado Shaibu.

Chanzo: Mwananchi