Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Tulia: Bunge 'Halitamezwa' na Serikali

Tulia (3) Spika Dk Tulia Ackson

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALIYEKUWA Naibu Spika Dk Tulia Ackson na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema Mhimili wa Bunge umepewa majukumu kikatiba kuisimamia na kuishauri serikali haijarishi ni wabunge wanatoka chama gani.

“Mbunge anapokuwa Bungeni ni mwakilishi wa wananchi. Hoja ya kwamba Bunge lina wabunge wengi wa CCM linaweza kumezwa na serikali huo uwezekano haupo kwa sababu serikali haiwezi kumeza Bunge na wala Bunge haliwezi kumeza Serikali.

“Serikali kazi yake ni utendaji na Bunge kazi yake ni kusimamia Serikali,” alisema Dk Tulia wakati akijibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM).

Gambo alidai katika swali lake kuwa Bunge lina wabunge wengi wa Chama tawala na hivyo ni rahisi kwa bunge kumezwa na kushindwa kukosoa na kusimamia serikali. “Tukikuchagua kuwa spika unatuhakikishiaje kulinda heshima na hadhi ya bunge ndani na nje ya Bunge?”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live