Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt Samizi CCM Ashinda Uchaguzi Muhambwe

Muhambwe?fit=680%2C453&ssl=1 Dkt Samizi CCM Ashinda Uchaguzi Muhambwe

Mon, 17 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MGOMBEA wa CCM katika jimbo la Muhambwe, Dk Florence Samizi ametangazwa mshindi katika uchaguzi ulifanyika jana. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Muhambwe, Atashasta Nditiye kufariki Feberuari mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 17, 2021 msimamizi wa uchaguzi, Diocles Rutema amesema Dk Samizi ameshinda kwa kupata kura 23,441 kati ya kura halali 34,656.

“Kwa mamlaka niliyopewa na kifungu cha 81 (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 443 ninamtangaza Dk Florence Samizi kuwa mbunge wa Muhambwe,” amesema Rutema.

Amebainisha wagombea wengine katika uchaguzi huo, Julius Masabo (ACT-Wazalendo) amepata kura 10,847 na Philipo Fumbo wa Democratic Party (DP) kura 368.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Dk Samizi ameahidi kuanza utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni baada ya kuapishwa.

“Kama nilivyosema wanikopeshe kura nami nitawalipa maendeleo, naamini baada ya hapa nitaanza utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo ndiyo inaniongoza utekelezaji wangu,” amesema Samizi.

Naye Fumbo amemuomba Dk Samizi kuwashirikisha washindani wake katika utekelezaji wa majukumu yake ndani ya jimbo hilo.

“Sisi tupo tayari kushirikiana naye hata kwa kumshauri sio vibaya kushirikiana na mshindani wako,” amesema Fumbo.

Fumbo amesema matokeo hayo yametangazwa kama yalivyokuwa yameandikwa kwenye vituo.

Mapema jana kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akimpongeza Dk Samizi kwa ushindi huo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz