Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mollel: CHADEMA wanaisema CCM wakati wanaishi nyumba ya kupanga

Mollell Ed Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri Afya

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Siha, Godwin Mollel ametema nyongo kwa wapinzani wenye tabia ya kutoa maneno ya kashfa kwa chama tawala cha CCM huku wakidai kuwa hakitimizi majukumu yake ya kujenga taifa ipasavyo na kuwataka wakae kimya kwani anayajua mengi yanayowahusu wapinzani.

Akizungumza na kituo cha redio cha Wasafi, Dkt.Mollel amesema kuwa aliona mengi wakati alipotimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, na kubainisha kuwa licha ya kuwa walikuwa wakipokea mabilioni ya fedha za Ruzuku lakini wengi wa viongozi wa chama hicho wanaishi nyumba za kupanga.

Ameongeza kusema kuwa kukashfu CCM kuwa haifanyi kazi wakati wapinzani hao wanashindwa kufanya maendeleo binafsi hai kufikia kuishi mazingira yasiyoendana na hadhi zao haitoi tafsri nzuri katika mlengo wa kisiasa.

"Nilikua mwenyekiti wa UVCCM 2008 - 2012 baadaye nikahamia Chadema, nikawa upinzani kwa wanaosema hakuna kilichofanywa na CCM na nilipokua nao niliona mengi. Wanapata mabilioni kutokana na ruzuku lakini mpaka leo wanaishi nyumba ya kupanga. Mtu anakwambia CCM haijafanya kitu ila yeye anashindwa hata kuweka kapeti sehemu anapoishi," - Dkt. Godwin Mollel, Mbunge wa Siha na Naibu waziri wa Afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live