Uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa utasimamiwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Uchaguzi huo unafanyika leo Jumapili Novemba 27, 2022 katika ukumbi wa Jiji uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Wajumbe wa mkutano Mkuu wa umoja huo wanatarajia kuwachagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, wajumbe wa watatu wa Halmashauri Kuu (NEC) kutoka Tanzania Bara na wawili Zanzibar, wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza katika mkutano huo, Dk Tulia amewataka wajumbe wa mkutano huo kuacha kampeni kwani muda umekwisha.
"Mnavyoimba hizo nyimbo mnaoneka kabisa mnafanyia kampeni acheni naombeni muwe na utulivu," amesema Dk Tulia.
Kauli hiyo ya Spika imekuja kufuatia wajumbe kila mara kutaja jina la mgombea aitwaye Mohammed Ali Mohammed (Kawaida)
"Kawaida Kawaida Kawaida Kawaida,"Wajumbe kila muda walikuwa wakiimba. Wagombea wengine katika nafasi ya Mwenyekiti ni Farid Mohammed Haji, Kassim Haji Kassu na Mohammed Ibrahim Natepe.
Kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti wagombea ni Khadija Ismail,Dorice Mgeta,Victoria Mwanziva na Rehema Omary