Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Tulia kutoa tuzo kwa walimu, wanafunzi mkoani Mbeya

92977 Pic+tulia Dk Tulia kutoa tuzo kwa walimu, wanafunzi mkoani Mbeya

Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Naibu Spika wa Tanzania, Dk Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust leo Ijumaa Januari 24, 2020 atatoa tuzo kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari mwaka 2019 mkoani Mbeya.

Tuzo hizo za Tulia Trust Education Awards zilianza kutolewa mwaka 2019.

Akizungumza leo meneja wa taasisi hiyo, Jackline Boaz amesema lengo la kutoa tuzo hizo ni kutoa hamasa na kupandisha kiwango cha elimu mkoani humo.

“Lengo la Tulia Trust ni kumfanya mwalimu ahamasike kufundisha kwa bidii, wanafunzi wasome  kwa bidii lakini shule inayofanya vizuri ipate sifa. Tunaamini huu ni mchango wetu kupandisha kiwango cha elimu kwa kutoa motisha kwa walimu, wanafunzi na shule bora.”

“Leo tunatoa printa saba kwa shule zilizofanya vizuri lakini zenye uhitaji, kwa upande wa walimu na wanafunzi watakaoibuka washindi watazawadiwa fedha taslimu na vyeti,” amesema.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Mbeya,  Fakhii Lulandala amesema kuanzishwa kwa tuzo hizo kumesaidia kupeleka faraja kwa walimu kuhamasika kufanya kazi kwa bidii.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz