Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Tulia aagiza Mchungaji Msigwa kuhojiwa kuthibitisha wizi wa kura uchaguzi mkuu 2015

83236 Tulia+pic Dk Tulia aagiza Mchungaji Msigwa kuhojiwa kuthibitisha wizi wa kura uchaguzi mkuu 2015

Sun, 10 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Naibu Spika wa Bunge la Tanzania,  Dk Tulia Ackson amemtaka mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa.

Amesema anatakiwa  kuthibitisha madai yake kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kura ziliibiwa.

Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba 6, 2019 baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama kuomba mwongozo akibainisha kuwa kauli aliyoitoa mbunge huyo inaonyesha  wabunge wote hawapo kihalali bungeni.

“Kauli hii inaonyesha kuwa uwepo wetu hapa sio halali jambo ambalo si sahihi na anavunja kanuni za Bunge, katiba na sheria,” amesema Mhagama.

Waziri huyo alimuomba Dk Tulia kumtaka mchungaji Msigwa kufuta kauli yake au kujikita kuzungumza jambo lililokuwa likijadiliwa bungeni.

Baada ya maelezo hayo ya Mhagama, naibu spika amemtaka mbunge huyo wa Iringa Mjini kufuta kauli yake  kabla ya Bunge kuangalia utaratibu mwingine. Katika majibu yake mchungaji Msigwa alisema katika jimbo la Kalambo kura ziliibiwa.

Wakati Dk Tulia akisisitiza kuwa amempa nafasi ya kufuta kauli yake au kutoa ushahidi, mbunge huyo alisema ana ushahidi kuwa kura ziliibiwa.

Kutokana na kauli yake hiyo alimtaka kufika mbele ya kamati hiyo kuthibitisha madai yake hayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz